Burudani ya Michezo Live

Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, arudi kwenye mpira na kulamba dili hili nono FIFA – Video

Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, arudi kwenye mpira na kulamba dili hili nono FIFA - Video

Kocha wa zamani wa Arsenal,Mfaransa Arsene Wenger, amelamba dili nono kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya Soka Duniani. (FIFA’s chief of global football development).Rais wa FIFA Gian Infantino amesema anaamini uzoefu na weledi wa Wenger utasaidia katika eneo la Ufundi na Utunzi wa sheria.
Hatua hiyo inamaliza uvumi wa kumuunganisha Mfaransa, 70, na kurudi kwa usimamizi kama bosi wa Bayern Munich.

Wenger aliondoka Gunners mnamo Mei 2018, baada ya kuhudumu kwa miaka 22, akishinda mataji matatu ya Ligi Kuu Uingereza na maKombe saba ya FA. Wenger amesema:-

“Ninachoangalia sana ni changamoto hii mpya na muhimu sana kwenye maisha yangu,”

Majukumu hayo mapya ya Wenger katika baraza linalotawala ulimwengu litasaidia kukuza mpira wa miguu wa wanaume na wanawake, na pia nyanja za kiufundi za mchezo huo.

Sasa atakuwa mwanachama wa jopo la kiufundi la Bodi ya Chama cha Soka la Kimataifa, na mwenyekiti wa bodi ya masomo ya kiufundi zaidi Fifa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW