Michezo

Kodi kumfukuza Ronaldo Hispania

Mchezaji wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, Cristiano Ronaldo ameonekana kukerekwa na tuhuma za udanganyifu wa ulipajikodi zinazoendelea nchini Hispania.

Mchezaji wa Real Madrid, Cristian Ronaldo

Mtu wa karibu wa mchezaji huyo ameliambia shirika la habari la BBC kuwa Ronaldo anafikiria kuondoka Madrid.
Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid akitokea Manchester United mwaka 2009 kwa dau la paundi milioni 80, mkataba wake unafikia euro bilioni moja (£874.88m)

Ligi ya China tayari imeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya Mreno huyo lakini washauri wake wakaribu wanapenda achezee Ulaya ama kwenda kukipiga katika klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa.

Ronaldo, ameisadia Real kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhuma za udanyafu wa ulipajikodi wa takribani euro 14.7m (£13m; $16m) kati ya mwaka 2011 na 2014.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents