Habari

Kodi mpya ya Ufaransa kwa makampuni ya Google, Amazon na Facebook yaishtua Marekani, yajipanga kulipiza kisasi

Utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani umependekeza ushuru wenye thamani ya dola bilioni 2.4 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Ufaransa kama jibini na mikoba ya wanawake, kulipiza kisasi hatua ya nchi hiyo kuyatoza kodi makampuni maarufu ya kidigitali kutoka Marekani, kama Google, Amazon na Facebook.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Deutsche Welle, Ofisi ya mwakilishi wa kibiashara wa Marekani imesema kodi hiyo mpya ya Ufaransa ilikuwa ikiyabagua makampuni ya kimarekani, na kuongeza kuwa ushuru utakaowekwa na nchi yake unaweza kufikia asilimia 100 ya thamani ya bidhaa za Ufaransa.

Ofisi hiyo imesema itasikiliza maoni ya umma wa Marekani kuhusu mpango wake, katika kikao kitakachofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 7 za mwezi ujao wa Januari.

Ufaransa imesema lengo la kodi yake ni kuyazuia makampuni hayo ya kimarekani kukwepa kodi kwa kuweka makao yake makuu katika nchi zenye viwango vya chini vya kodi barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents