Habari

Koffi Olomide ahukumiwa kifungo cha miezi mitatu ‘kilichotenguliwa’


Mwanamuziki wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela ambacho hata hivyo hatakitumikia.
Kifungo hicho kijulikanacho kisheria kama ‘suspended prison sentence’ amekipata baada ya kumjeruhi producer wake.
Kifungo hicho kinamaanisha kuwa atakuwa chini ya uangalizi ambapo kama ataonesha tabia njema na kuzingatia masharti aliyopewa, kifungo hicho hufutwa kabisa.
Hata hivyo producer huyo alitaka kuiondoa kesi hiyo mahakamani ili wayamalize kindugu na Koffi ambaye anamuita ‘kaka mkubwa’.
Ugomvi huo ulitokea kwenye hoteli moja mjini Kinshasa ambapo producer wa Koffi , Diego Lubaki, alikuwa ameutembelea mji huo kwa siku chache.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mwanamuziki huyo alienda kwenye hoteli aliyofikia producer ajulikanaye zaidi kama “Diego Music” na kuzuka ugomvi. Koffi alitaka wajadiliane kuhusiana na fedha aliyokuwa amemlipa ili amfanyie video ambayo hata hivyo haikufanyika.
Nyota hao walijikuta wakizichapa na ndipo walinzi wa hoteli hiyo kuingilia na Koffi alikamatwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents