Habari

Koffi Olomide ahukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la unyanyasaji wanawake kingono na ubakaji

Msanii wa muziki mkongwe nchini DR Congo, Koffi Olomidé, amehukumiwa miaka miwili jela au kulipa faini ya Euro 5,000 baada ya kukutwa na hatia ya unyanyasaji kingono na ubakaji kwa moja ya waliokuwa Dancers wake miaka 15 iliyopita.

Koffi Olomide

Hukumu hiyo imetolewa jana na mahakama ya Nanterre mjini Paris, Ufaransa.

Hata hivyo, wakati wa hukumu hiyo inasomwa, Koffi Olomide hakuwepo mahakamani hapo.

Olomidé, mwenye umri wa miaka 62, ametakiwa alipe Euro 5,000 kwa madhara aliyomsababishia mwanamke huyo.

Wakili wa Olomidé amepongeza uamuzi huo na kuutaja kuwa ushindi, akiwaarifu waandishi habari kwamba uamuzi huo utachangia kuondolewa waranti wa kimataifa wa kumkamata.

Koffi Olomidé ni nyota wa muziki wa mtindo wa rumba na soukous ambao ni maarufu sana barani Afrika.

Mwaka 2012, Olomidé alishtakiwa kwa mara ya kwanza kwa makosa ya ubakaji na unyanyasaji kingono, lakini alikana makosa yote.

Imeelezwa kuwa Olomide aliwanyanyasa kingono wanenguaji wake wanne kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006 nchini DR Congo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents