Habari

Koffi Olomide awashauri wanamuziki wa Tanzania kujiamini

Mwanamuziki kutoka DRC Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kwa jina la Koffi Olomide ambaye yupo nchini, amewashauri wasanii wa Tanzania kujiamini ili waweze kufanikiwa kimataifa.

Koffi ametoa ushauri huo katika mahojiano ya moja kwa moja yaliyofanyika leo jioni kupitia Clouds TV.

Amesema ili wasanii hao waweze kuchana mbuga zaidi wanatakiwa kujiamini kwa kile wanachokifanya na kusema kuwa amekuwa akisikia kazi nyingi za wasanii wa Tanzania.

Alipoulizwa kuhusu kudaiwa kuwepo kwa beef kati yake na Felix Wazekwa, mwanamuziki huyo ambaye ni msomi wa masters ya hesabu aliyoipata nchini Ufaransa amesema hana beef na msanii huyo na wala hana muda wa kujihusisha na uadui na msanii yeyote zaidi ya kazi.

Kesho anatarajia kufanya show katika viwanja vya Leaders Club.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents