Burudani

Kofia ya Pharrell Williams iliyopigwa mnada yanunuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 70

Producer na mwimbaji Pharrell Williams wiki iliyopita aliipiga mnada kofia yake maarufu (buffalo hat) aliyoivaa katika tuzo za Grammy, kama njia ya kukusanya pesa kwaajili ya mradi wa kusaidia vijana walio katika hatari (From One Hand to Another).

Pharrell Grammy

Mshindi katika mnada huo kupitia ebay ni mgahawa wa Arby’s ambao wameinunua kwa dola 44,100 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 70 za Tanzania.

arb

“Thank you to whoever bought my Grammy hat on @eBay for $44,100,Your donation benefits From One Hand to Another.” Alitweet Pharrell baada ya kofia kununuliwa.

aaa

Logo ya mgahawa huo inamchoro unaofanana na kofia iliyokuwa ya Williams.

Arby’s walioinunua kofia hiyo nao walijibu:
“You’re welcome. We’re HAPPY to support a great cause & get our hat back. Good luck at the #Oscars tonight!”

Pharrell Oscar

Katika Tuzo za Oscar zilizofanyika Jumapili iliyopita Williams aliperform hit song yake ‘Happy’ huku akiwa amevaa version ingine ya kofia kama ile aliyoipiga mnada.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents