Kolabo na Khaligraph Jones yamsikitisha Young Killer

Msanii wa muziki Bongo, Young Killer amesema amesikitishwa na kitendo cha kolabo yake na Khaligraph Jones kuvuja.

Rapper huyo ameiambia 5 Selekt ya EATV kuwa ngoma hiyo ilikuwa kwenye mipango mikubwa ambayo si kwa wakati huu.

“Napenda kusikitika na kutoa taarifa hizi rasmi kutokana na wimbo ambao nimefanya Khaligraph Jones kuwa umevuja ni kitu ambacho mwenyewe kimenishangaza hata Khaligraph mwenyewe kanicheki kiukweli kwa namna moja au nyingine imeni- disappoint,” amesema.

“Sijui imetoka kwa mazingira gani kwa style gani kwa sababu ni wimbo ulikuwa na mipango mikubwa, ilikuwa ni demo imekuja katika wakati ambao sio,” amesisitiza.

Ngoma ambayo Young Killer anadai imevuja inakwenda kwa jina la How we Do.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW