Burudani

Kolabo ya Drake na The Weeknd mbioni kuja

Boss wa OVO Sound, Drake anatarajia kuachia ngoma yake mpya wakati wowote. Hii imekuja baada ya rapper huyo kuweka picha akiwa studio katika mtandoa wa kijamii.

Picha hiyo iliwekwa na Drake siku ya jana (Jumapili) katika mtandao wa Instagram yenye kuashiria  anaingiza sauti kwa ajili ya ngoma yake mpya ambayo inahisiwa kuwa ndiyo ile aliyotoa ahadi  atafanya na The Weeknd.

https://www.instagram.com/p/BY4j3dhjLKr/?taken-by=champagnepapi

Mwezi uliopita katika tamasha la OVO la rapper huyo aliahidi mashabiki zake kuwa ataungana na The Weeknd katika albamu ijayo. ” I want you to understand what this is. First of all, i dont want to do this to you on stage, buyt i feel like that OVOXO project has to happen at some point. I just want say that,” alisema Drake wakati wa tamasha hilo mwezi uliopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents