Kongamano la Kiswahili lasisitiza umuhimu wa kuikuza lugha hiyo
Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Susan Kolimba,amewataka wataalamu wa lugha ya Kiswahili kuendelea kukuza lugha hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Ameyasema hayo katika kongamano la chama cha Kiswahili la Afrika, lilifanyika katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, alipokuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo.
“Nawapongeza kwa jihihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, katika kuikuza lugha ya Kiswahili, niwaombe wataalam wa lugha ya Kiswahili kuchangamkia fursa za fani hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki,” alisema Kolimba.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi za Afrika Mashariki, mabalozi,wabunge, na balozi wa Kiswahili Afrika ambaye ni mke wa rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete.
BY: EMMY MWAIPOPO