Habari

Kontena 10 za kemikali bashirifu zakamatwa Dar

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imekamata makontena 10 yenye lita 200,000 za kemikali bashrifu katika Bandari ya Dar es Salaam ambazo zimeingizwa kutoka nchini Swaziland kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, imebaini kuwa kampuni inayotuhumiwa kwa sakata hilo imekuwa ikiingiza kemikali hizo tangu mwaka 2016, ambapo taarifa zinaonyesha waliwahi kuingiza lita milioni 1.5 za kemikali bashirifu ambazo zinaonyesha zilipelekwa kwenye kampuni moja iliyoko Mbezi Luis.

Baada ya kufuatilia wakagundua kuwa kampuni hiyo inajihusisha na yard ya magari na siyo kutunza wala kuchakata kemikali jambao ambalo liliwapa wasiwasi na kuamua kufanya uchunguzi zaidi.

Source: Globalpublishers

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents