Habari

Kora Awards 2012: Chris Brown agoma kuperform, waandaaji walaumiwa kwa kutojipanga

Chris+Brown+New+York+Knicks+v+Los+Angeles+SGpYZxN7G7il

Zikikumbwa na matatizo kibao ya kiuandaaji, tuzo za Kora 2012 hatimaye zilifanyika jana Jumapili.Kora iliahirishwa kufanyika Jumamosi kutokana na kuchelewa kuwasili vyombo muhimu.

Sababu nyingine ni kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa iliyowapa shida mafundi mitambo kuweka mambo sawa.Chris Brown na Rihanna waliwasili jana jioni na Chris kutumbuiza kwenye uwanja wa Houphouet-Boigny wa mjini Abidjan nchini Ivory Coast katika tamasha la Amani lakini hata hivyo hakuhudhuria utoaji wa tuzo ambako alikuwa amepangwa kuimba.

Awali Chris alikuwa pia amegoma kutumbuiza uwanjani hapo baada ya kuona nusu ya uwanja haina watu.Kutokana na mahudhurio hafifu uwanjani hapo waandaji waliamua kushusha bei ya kiingilio kabla ya kuondoa kabisa na kuwa bure lakini hata hivyo uwanja huo haukujaa.

Pamoja na matatizo ya mwisho mwisho ya kiuandaaji tuzo hizo ziliingiwa na dosari kutokana na kiingilio chake kuwa kikubwa kulingana na maisha ya wananchi wan chi hiyo ambapo kilikuwa ni euro 1,500 (zaidi ya shilingi 350,000 za kitanzania). Hali hiyo ilipelekea baadhi ya meza kubaki tupu.

Waandaaji walilazimika kuomba radhi kwa makosa hayo ambapo mratibu mkuu Yves Zogbo alisema, “ The Kora come a long way. I hope that the next edition will, through the one we just witnessed, reposition the event. Life is made of ups and downs, but we must learn. I am satisfied.”

Mpaka sasa hakuna list kamili ya washindi wa tuzo hizo za jana.Hata hivyo kundi la Magic System liliibuka washindi katika kipengele cha kundi bora la kiafrika la mwaka huku wasanii wa Nigeria kama Davido na Chidinma nao wakipata tuzo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents