Uncategorized

Korea Kaskazini kujiandaa kurusha makombora, picha za Satellite zanasa kinachoendelea, Rais Trump atoa neno

Picha za Satellite kutoka kituo kimoja karibu na mji wa Pyongyang zinashiria kuwa Korea Kaskazini inajiandaa ‘kurusha kombora’ ama roketi.

Kumeripotiwa shughuli nyingi katika eneo linalofahamika kama Sanumdong, ambapo Korea Kaskazini huunganishia makombora na maroketi yake.

Mapema wiki hii ripoti ziliibuka kuwa Korea Kaskazini imejenga kituo kikuu cha kikuu cha kuundia silaha zake za nuklia.

Shughuli ya kubomoa kituo cha Sohae ilianza mwaka jana lakini ikasitishwa baada ya mazungumzo kati ya marais Kim Jong un na Donald Trump kuvunjika.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Siku ya Ijumaa rais Trump alisema atasikitika sana ikiwa Korea Kaskazini itarejelea tena kufanyia majaribio silaha zake hatari.

Picha rasmi ya (KCNA) inaonesha Kiongozi wa Korea kaskazini na Kim Jong Un (kulia)na rais wa MarekaniDonald J. Trump (kushoto) wakikutana mjini Hanoi, Vietnam, Februari 28 2019.
Rais Trump amesema “Nitasikitika sana Korea Kaskazini wakifanyia majaribio silaha zao.”

“Nitasikitika sana kuona wakifanyia majaribio silaha zao.” alisema

Nini kinafanyika Sanumdong?

Magari makubwa yameonekana yakizunguka kituo cha silaha cha Sanumdong, hali ambayo siku zilizopita ziliashiriria kuwa Korea Kaskazini ilikuwa ikijiandaa kufyetua Kombora ama roketi kutoka eneo hilo.

Picha za satellite zimechapishwa na mitambo maalum ya Marekani inayofahamika kama NPR.

Mwandishi wa BBC mjini correspondent Laura Bicker amesema Korea Kaskazini huenda akaamua kuchukua hatua hiyo baada ya mazungumzo ya Hanoi kati ya Donald Trump na Kim Jong-un kumalizika bila kufikia muafaka wowote.

Ameongeza kuwa wataalamu wanahofia mitambo inayotumiwa kurusha silaha hizo hatari sio hasa kwa makombora ya masafa marefu.

Kulikuwa na matumaini kuwa viongozi hao wangelifikia mkataba wa kumaliza mzozo kati yao japo Korea Kaskazini ilikuwa tayari kupunguza shughuli zake za nuklia ikiwa Marekani ingeliondolea baadhi ya vikwazo dhidi yake.Mazungumzo ya Trump na Kim yavunjika bila muafaka

Kituo cha kurusha makombora cha Sohae Tongchang-ri kimetumiwa kufanyia majaribio baadhi ya silaha zake lakini siyo makombora ya masafa marefu.

Wiki hii picha za satellite, kutoka vituo kadhaa vya Marekani na pamoja na ushahidi kutoka shirika la kijasusi la Korea Kusini, zilionesha ujenzi upya katika mitambo ya kurusha maroketi.

Maafisa wa ulinzi wa Korea Kaskazini katika kituo cha Sohae (2012)

Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama nchini Marekani John Bolton, amesema kuwa Korea Kaskazini huenda ikawekewa vikwazo zaidi ikiwa itaendelea na mpango wake wa Nuklia.

Mkutano wa kwanza wa kihistoria kati ya Trump na Kim uliyofanyika mwaka 2018 nchini Singapore ulitoa matumaini ya uwezekano wa kukomesha mzozo katika rasi ya Korea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents