Habari

Korea Kaskazini watishia kuvunja mkutano wa Kim Jong-un na Trump

Huenda mkutano wa Rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi Kim Jong-un wa Korea Kaskazini usifanyike tene.

Taarifa hiyo imetolewa na Korea Kaskazini kwa madai iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia.

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini (KCNA) limemnukuu Naibu Waziri wa mambo ya nje, Kim Kye-gwan akisema kuwa “sharti hilo litawabana wao hivyo hawatakuwa tena na hamu ya kushiriki mazungumzo hayo na itawalazimu kutafakari upya iwapo watakubali mkutano huo.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumanne ya Juni 12, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents