Korea Kaskazini yadaiwa kuachana na mpango wa mazungumzo na Washington

Korea Kaskazini imesema kwamba haina mpango wa kuendelea na mazungumzo kuhusu nyuklia, hadi pale Marekani itakapochukua hatua za kumaliza mvutano.

North Korea, north korea US talks, Washington, Pyongyang, Sweden, DPRK counterparts

Nchi hiyo inaarifu hayo siku moja tangu kuvunjika kwa mazungumzo na Marekani yaliyosimamiwa na Sweden baada ya Pyongyang kuituhumu Washington kwa kutobadili msimamo wake kuelekea nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kaskazini amenukuliwa siku ya Jumamosi akisema Pyongyang, haitorejea kwenye meza ya majadiliano ya maudhi hadi Marekani itakapotekeleza hatua za kuachana na sera zake za uadui.

Shirika rasmi la habari la serikali ya Korea Kaskazini limemnukuu afisa huyo akisema, mustakabali wa mazungumzo hayo upo mikononi mwa Washington na kuongeza kuwa utekelezaji wake utahitimishwa mwishoni mwa mwaka huu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW