Habari

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu Japan

Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.

Kombora hilo lilirushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za jeshi la Korea kusini.

Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan.

Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika meizi ya hivi karibuni hatua inayoendelea kuzua wasiwasi.

Kombora hilo la siku ya Jumanne lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40,kulingana na Korea Kusini na Japan.

Hili ni kombora la 11 lililogunduliwa mwaka huu lakini urefu wake umeongezeka kulingana na mwandishi wa BBC mjini Seoul Stephens Evans.

Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mnamo mwezi Mei.

Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.

Waziri anayesimamia maswala ya serikali nchini humo Yoshihide Suga aliambia maripota:Uchokozi kama huu wa Korea kaskazini hauwezi kukubalika.Tuliwasilisha malalamishi yetu na kushutumu hatua hiyo.

Rais mpya wa Korea Kusini aliyechaguliwa hivi majuzi ametaka kufanywa kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la taifa hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents