Technology

Korea Kaskazini yazindua kombora jipya ‘linarushwa kutoka kwenye manowari (+ Video)

Taifa la Korea Kaskazini limezindua kombora jipya la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka kwa manowari. vyombo vya habari vya taifa hilo vimelielezea kuwa Hilo ni kombora lenye uwezo mkubwa duniani’.

Makombora kadhaa ya aina hiyo yalioneshwa katika gwaride la kijeshi lililosimamiwa na rais Kim Jong un, viliripoti vyombo vya vya habari vya taifa hilo.

Hatua hiyo inajiri kufuatia mkutano wa kisiasa usio wa kawaida ambapo bwana Kim aliitaja Marekani kama ‘adui yake mkubwa zaidi’.

Onesho hilo la uwezo wa kijeshi linajiri siku chache kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden kuwa rais.

Picha zilizotolewa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini zilionesha makombora manne makubwa yenye rangi nyeusi na nyeupe yakiendeshwa na kupitishwa mbele ya rais huyo huku kundi kubwa la watu likipunga mkono.

Wachambuzi wanasema kwamba ni kombora ambalo lilikuwa limefichwa.

Mwaka Mpya kombora jipya la Pukguksong,”Mtaalamu wa Korea kazkazini Ankit Panda, akitumia jina la kombora jipya linaloweza kurushwa kutoka kwa (SLBMs).

Akiwa amevalia koti na kofia, bwana Kim amepigwa picha akitabasamu na kupunga mkono huku akitazama onesho hilo katika bustani ya Kim Il Sung Square iliopo Pyongyang ambalo pia lilishirikisha wanajeshi wa vitengo mbali mbali, silaha na mizinga.

Kim Jong-un akiwa katika gwaride hilo la kijeshi
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisimamia onesho hilo la uwezo wa kijeshi

”Kombora hilo lenye uwezo mkubwa duniani , manuwari inayoweza kurusha kombora la masafa marefu ziliingia katika bustani hiyo zikifuatana , likionesha kwa kishindo kikubwa uwezo wa jeshi la taifa hilo”, kilisema chombo cha habari cha Korean Central News Agency said.

Bofya hapa chini:

https://www.instagram.com/tv/CKDwXSZhJjb/

https://www.instagram.com/tv/CKDwXSZhJjb/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents