Michezo

Ksh 450,000 zachangwa kumsaidia Conjestina (bondia wa kike wa Kenya aliyewehuka)


Jumla ya shilingi 450,000 za Kenya jana zimechangwa kwenye hafla ya kuchangisha fedha maalumu za kumsaidia bondia maarufu wa kike nchini Kenya, Conjestina Achieng aliyewehuka.

Kampeni ya kumchangishia fedha Conje ilianzishwa na rapper Nonini aliyekuwa akishirikiana na mchekeshaji Churchill, blogger Robert Alai na balozi Yvonne Khamati.

Nonini, ambaye alifurahishwa na muitikio mkubwa wa watu katika kumchangia bondia huyo, alisema kuwa Conjestina hakuifurahisha Kenya pekee bali dunia nzima hivyo anatakiwa kusaidiwa arudi ulingoni tena.

Aliwakumbusha pia wakenya kuwa hawatakiwi kutegemea serikali katika kila jambo.

Miongoni wa wachangiaji waliotia fora ni pamoja na mbunge wa Makadara, Mike Sonko aliyetoa shilingi 50,000 za Kenya pia aliahidi kumlipia ada mtoto wa kiume wa Conje na kumnunulia seti ya sofa.

Tukio hilo lilihudhuriwa na watu maarufu wakiwemo aliyekuwa mshiriki wa TPF Wendy Kimani, Nameless na mke wake Wahu, Suzanna Owiyo, Jua Cali, Big Ted na DJ Creme de la Crème.

Conjestina ambaye alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya magonjwa ya akili ya Mathari Mental leo atahamishiwa Chiromo Lane.
Resolution Health imeahidi kulipia matibabu ya Conjestina na mwanae kwa mwaka mzima na kuchangia shilingi 100,000.

The Yvonne Khamati Foundation itamwajiri nesi wa kumhudumia Conjestina pindi atakapotoka hospitali ambaye atamwangalia kwa miezi sita na pia itamlipia ada ya kozi ya Diploma ya saikolojia ya michezo na ushauri nasaha kwenye chuo cha Eden Therapy.

Shirika la Basics Needs United Kingdom litatoa ushauri nasaha kwa dada yake Conjestina, Carol na mwanae, wakati kampuni ya Blackberry Kenya ikiahidi kuiwekea furniture nyumba atakayohamia Conjestina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents