Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Kuanguka kwa Jengo Dar: MwanaFA, Profesa Jay, Vanessa Mdee, Lady Jaydee, Grace Matata na wengine waongea

Mastaa mbalimbali nchini wameungana na wananchi wengine wa jijini Dar es Salaam kuombeleza vifo vya watu ambao bado idadi yao kamili haijajulikana waliopoteza maisha leo asubuhi baada ya jengo lenye ghorofa takriban 15 kuanguka katika ya jiji hilo.

IMG-20130329-WA002

Jengo hilo lilikuwa likiendelea kujengwa na taarifa za awali zinadai kuwa karibu watu 60 wanahofiwa kupoteza maisha na shughuli za uokoaji na kuondoa vifusi ikiendelea.

Haya ni maoni ya baadhi ya mastaa na viongozi wa Tanzania walioguswa na tukio hilo:

Rais Jakaya Kikwete

Dua zangu kwa Watanzania wenzetu waliokumbwa na maafa ya kuanguka kwa jengo eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam asubuhi yao leo. Undugu na umoja usiojali tofauti yoyote unaojionyesha katika shughuli za uokoaji zinazoendelea ni jambo la faraja na la kutia moyo sana.

Mwana FA

Sio mara ya kwanza,hatujifunzi kitu aunty..uzembe wa mijitu mipuuzi unaangamiza maisha ya watu..na bado wanajenga.

Ben Pol

My heart goes out to all those who have lost their loved ones in the fallen building in the City Centre. So so sad. #Inasikitishasana.

Salama A. Jabir

Mwenyezi Awalaze Pema Walopoteza Maisha Leo Kwenye Jengo Lilodondoka…Matumaini Yangu Tumejifunza Kitu. Insha’Allah Kheri.

Joseph Haule ‏

Haya majengo yanayoota mjini kama UYOGA inabidi yaangaliwe sana ubora wake, la sivyo tutazidi kupoteza Ndugu zetu kila Kukicha! POLENI WOTE.

Grace Matata ‏

Now we got buildings crumbling kama utani. Hii nchi, mweeeee…. Dah, hapa kila jengo ntakaloingia ntakuwa najiuliza mara mbili mbili. Kazi kweli kweli ndugu yangu.

Allan Lucky‏

Kuna jengo lipo katikati ya jiji kabisa, nina wasi wasi ipo siku litaporomoka. Mi sio mkandarasi, but naliogopa! Watu wa viwango mko wapi?

Lady JayDee‏

Hivi hizi habari huwa zinatokaje, Mara ghorofa 17, 12, 16 mara 15? Tuelewe lipi? Hakuna mwenye uhakika ina maana? Mmhh!! Poleni wafiwa

Arnold Kayanda

Nawatakia kupona haraka walioumia,Mungu awarehemu waliofariki! Natoa pongezi kwa wote wanaoshiriki katika uokoaji!

Vanessa Mdee

Saddened by the news of this sudden collapse of a building in the city centre. Thoughts n prayers to the families who’ve lost loved ones.

Tayana S Tibenda

Inasikitisha sana tamaa ya hela unaua watanzania?!!?? Huyu mwenye hili gorofa lililoangua leo posta afungwe..mxxiiiiiiii kabisa. More sad watoto maskini waliopoteza maisha yao!

Maua Sama‏

RIp to those hu died in the accident ..!! NA Mungu awaponye wale majeruhi..Ameen!

Bernard Membe

Nimesikitishwa na taarifa za ajali na vifo kutokana na kuanguka kwa jengo.Natoa pole kwa wafiwa na majeruhi,uongozi wa mkoa na @JerrySilaa

January Makamba‏

My TL on collapsed building: only few are praying for the victims. Only one inquired about contributing to rescue efforts. Blame dominates.

Mwezi uliopita jengo lenye ghorofa nne jijini Dar es Salaam lilianguka na kusababisha kifo cha mtoto mmoja aliyekuwa na umri kati ya mika 10 hadi 11.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW