Habari

Kuanzisha jambo ni rahisi lakini kuendeleza kunahitaji ujasiri

Kwenye mazingira ya taharuki kubwa wakati vitu vingi vikiwa kwenye maswali mengi, huwa nashangaa kama haya yote ya kutojiamini na kuchanganyikiwa kama yana thamani ya kupoteza kile nilichokiacha.

plumbers-X2

“Je kwanini nisirudi nyuma nikakichukue? Au kwanini nisiirudie ile kazi ambayo ilinisaidia kulipa ada na pango la nyumba ninayoishi? Kwanini nisirudi tu kule niendelee kuweka heshima mjini?” ni kauli ya mmoja wa watu ambaye alijiuliza na mwisho wa siku akasema leo naaamua kuacha kazi.

Nilichojifunza kwa mtu huyo anasema ujasiri unaohitajika unabakia ndani ya mtu bila kutikiswa na jambo lolote katika pilika pilika za maisha ya kila siku na kufanya uendelee mbele bila kuchoka.

Bwana Machael anasema kwa miaka minne ambayo alikuwa hafanyi kazi ofisini, hamfanyii kazi mtu yeyote na wala hakuwa na kipato cha kutegemewa ambacho kingempa ujasiri hata akiumwa au kupata dharura kiweze kumsaidia. Anasema alijifunza vitu vingi kuhusu yeye mwenyewe na inawezekana asingeweza kujifunza hivyo kama asingepitia kipindi hicho.  “Ukweli wa mambo nikagundua woga, hofu na mashaka ni kitu halisi kabisa na tunakumbana navyo kila siku tunapoamka,” anasema,

Woga huchukua sura fulani hivi na inaweza kukuendesha kuelekea sehemu yoyote. Hujidhihirisha kwa kimo cha mafanikio katika kipindi chako cha kushindwa. Kabla ya hapo niliweza kuongelea kuhusu ujasiriamali, na kusema kwamba wajasiriamali si kwamba wameshinda woga bali wanaweza kukabiliana nao kila siku.

Kuna wengine wamesema, “Kinachojalisha ni ujasiri wa kuendelea tu.” Hii inamaanisha usianzishe kitu halafu ukaishia njiani. Wewe utakuwa huna ujasiri huo maana umekimbia vita. Watu waoga ni vigumu sana kuendelea na jambo kwani wao wanafikiri mafanikio huja kirahisi rahisi, Unahitaji ujasiri wa kuendelea kufanya jambo ili ufikie malengo yako uliyojiwekea na wala hakuna njia ya mkato katika kufanikiwa.

Unachohitaji ni kujifunza mwenendo mzima wa soko kama unaingia kwenye biashara na ujue kuna wakati mambo hayataenda unavyodhani. Hivyo unatakiwa kujiandaa kisaikolojia kujua maisha ya kibiashara kabla ya kuingia huko.

Ujasiri sio kufanya mambo bila kufikiri bali kuangalia uwezekano ambao utakuwa mkubwa wa wewe kushinda kuliko kushindwa. Inakubidi uwe na mapafu ya kuhakikisha mambo yanakweda sawasawa na kuongeza ushawishi wa mawazo, mbinu na ujuzi ili kuweza kusogeza gurudumu hilo.

Kama ukiweza kuanzisha kitu na wala hakuna anayekusifu wewe endelea tu kama hicho kitu ni halali au hata kama ni bidhaa watu wanaweza wasielewe leo lakini baadaye wakaelewa kama ulifanya uchunguzi wa kina wa kitu unachokitengeneza.

Ukiweza kuendelea huo ni ujasiri bila kujali vikwazo katika kila unachokifanya lazima utafika sehemu ambayo itakupa mafanikio makubwa.

Anza kidogo kidogo bila makuu ili upate nguvu ya kuendeleza hicho kitu kila siku. Mara nyingine hakuna mtiririko maalumu wa kuendelea kama unafanya vitu vya msingi na umejenga msingi wa kitaaluma na kibiashara mambo mengine uzoefu na kujifunza kutakupa mbinu mpya kila siku za kukusaidia kusongoa mbele.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents