Tupo Nawe

DERBY ya jiji la Dar, kiongozi wa Simba asisitiza pointi tatu ni muhimu, Mtendaji Mkuu wa Azam FC akiri wao ni ‘underdog’ mbele ya Mnyama

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba SC hii leo wanatarajia kushuka kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaama kuwakabili waoka mikate wa Chamazi, Azam FC wakiwa kama wageni.

Kuelekea mchezo Meneja wa Simba SC, Patrick Rweyemamu amefanya mazungumzo na radio EFM kabla ya mechi yao.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amezungumzia juu ya kikosi chao ”Wachezaji wapo kamili, kimwili na kiakili na tupo tayari kwa mpambano.”

Patrick Rweyemamu ameongeza ”Wachezaji wote wapo salama, tunawaheshimu Azam na timu zote zilizopo Primier League, tutaingia kwa tahadhari kubwa katika kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu katika kuelekea kutetea ubingwa wetu.”

”Ratiba ni ngumu lakini mwisho wa siku tupo kwenye ligi lazima tupambane, kwa hiyo sisi tupo tayari kwaajili ya mapambano, wachezaji na viongozi wanatambua hilo.”

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alikuwa na kauli hii kuelekea katika mtanange huo ” Azam tupo vizuri kuelekea kwenye mechi hiyo, timu hizi mbili zikikutana inakuwa mechi kubwa.”

”Simba ni timu kubwa tunaiheshimu, tunajua uwezo wao na wana timu bora ukilingana na sisi.”

”Sisi tunaingia kama ‘underdog’ kwasababu sisi ni wadogo siku zote kwa Simba na Yanga lakini tunaenda kupambana na hata wao wenyewe wanaelewa kama Azam ni timu ya haina gani na tunapokutananao wenyewe wanafahamu mechi inakuwa ya haina gani.”

”Tunaomba mechi iwe faer tu kwa waamuzi maana marefa rii ndiyo wanaweza kuamua mchezo huwe mzuri au mbaya.”

Kabla ya kukutana hii leo, haya ndiyo matokeo ya mechi zilizopita wakiwa wamtoka sare mara sita (6), Simba ikishinda mara tisa (9) wakati kwa upande wa Azam FC ikishinda mara tano (5).

2008/2009
Simba 0-2 azam
Azam 0-3 simba

2009/2010
Simba 1-0 Azam
Azam 0-2 Simba

2010/2011
Azam 1-2 Simba
Simba 2-3 Azam

2011/2012
Azam 0-0 Simba
Simba 2-0 Azam

2012/2013

Simba 3-1 Azam
Azam 2-2 Simba

2013/2014
Simba 1-2 Azam
Azam 2-1 Simba

2014/2015
Azam 1-1 Simba
Simba 2-1 Azam

2015/2016
Azam 2-2 Simba
Simba 0-0 Azam

2016/2017
Azam 0-1 Simba
Simba 0-1 Azam

2017/2018
Azam 0-0 Simba
Simba 1-0 Azam

Simba win-9
Azam win-5
Draw-6

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW