Michezo

Kuelekea fainali ya Europa: Klabu ya Arsenal yapatwa na pigo, Chelsea mwendo mdundo

Kutokana na sababu za kiusalama, Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kuwa haitamjumuisha kiungo wao mshambuliaji, Henrikh Mkhitaryan kwenye kikosi kitakacho safiri kwenda mjini Baku nchini Azerbaijan kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Europa unaotarajiwa kuchezwa tarehe 29 mwezi huu.

Image result for Henrikh Mkhitaryan

Arsenal imetoa taarifa hiyo rasmi, ikieleza kuwa sababu za kiusalama kwa, Muarmenia Mkhitaryan ndio zimepelekea kumtoa kwenye kikosi.

Tayari shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) wameshajibu maombi ya Arsenal na limeeleza kuwa maombi hayo ni ya sababu za mtu binafsi hivyo wamemkubalia bila hiyana.

Sababu kubwa ya Mkhitaryan ambaye ni raia wa Armenia kutokwenda nchini Azerbaijan ni kutokana na uhasama wa toka enzi kati ya mataifa hayo madogo kabisa barani Ulaya.

Wakati Arsenal wakitangaza pigo hilo, kwa upande wa wapinzani wao Chelsea hao wanaendelea vizuri ambapo hadi sasa hakuna taarifa yeyote mbaya ya majeruhi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents