Burudani ya Michezo Live

Kuelekea Valentines Day: Kumpata mpenzi anayekufaa fanya haya kwa wakati sahihi

Karibu kila weekend … katika jamvi lako la Love Bite kwa ajili ya kuelimishana mambo mbalimbali kuhusu mapenzi. Watu wengi wanaumizwa, wanateswa na mapenzi au wapenzi wao na wanashindwa kuendelea na maisha mengine kwa kuamini kuwa hakuna maisha nje ya maumivu ya mapenzi. Bongo Love itakuwa nafasi ya kuweza kupata makala, ushauri na maswali mbalimbali kuhusu mapenzi.

Umeishahi kujiuliza kama unahitaji mpenzi anayekufaa kwenye maisha yako, wewe mwenyewe unatakiwa uweje? Maana haiwezekani wewe unayetaka mwanamke au mwanaume anayekufaa lakini wewe mwenyewe ni kicheche, hujatulia, kila kukicha unarukaruka mara huku mara kule.

Siku lazika kuwa na uwiano wa baadhi ya mambo katika kumtafuta mpenzi wako ambaye unatamani awe mke au mumeo.

Kabla ya kuanza kumsaka mpenzi anayekufaa, yakupasa kujiuliza je, wewe ni mwanaume au mwanamke mwenye mambo yafuatayo:

UNA NIA YA DHATI

Kwa jambo ambalo umefikia kulifanya, je, ni kweli una nia ya dhati au unataka kufanya kwa sababu wengine wanafanya au unataka kuoa au kuolewa kwa sababu uliosoma nao wameoa au kuolewa sana.

Katika suala la kumtafuta anayekufaa lazima ujiulize juu ya nia ya dhati yaw ewe kumtafuta mpenzi uliyemlenga.

JE, UNAJITAMBUA?

Swali la kwanza kwako lazima liwe, je, wewe mwenyewe unayetaka anayekufaa, binafsi unajitambua kama mwanamke au mwanaume mwenye thamani kwa yule unayemuhitaji? Au unataka kumuoa au kuolewa ili ukawe pasua kichwa kwa mwenzako.

JE, WEWE SI MAPEPE?

Kuna maswali mengine yanakukugusa lakini lazima ujiulize ili kujifahamu kabla ya kuingia kwenye ndoa. Maana usiwe unataka mke au mume anayefaa wakati wewe mwenyewe ni mapepe uliyeshindikana. Hakuna mzazi mtaani ambaye yuko tayari kuona mwanaye anakuoa au anaolewa nawe kwa sababu ya tabia zako.

UNAHESHIMA?

Kabla ya kutaka mwanamke au mwanaume ambaye atakuheshimu kama mke au mume je, wewe mwenyewe unaujiheshimu?

Huna sababu ya kulazimisha kupata mpenzi anatakayekuheshimu wakati wewe mwenyewe hujiheshimu, mambo na vitu unavyovifanya haviendani na muonekano wako.

UNAJILINDA

Lazima wewe mwenyewe ujilinde kwanza ndipo mwenza wako apate nafasi ya kukulianda, unajilinda kwa sababu mtu wa kwanza kwenye maamuzi mabaya au mazuri ni wewe mwenyewe. Hivyo lazima uwe na uhakika kama wewe ni mtu wa kujilinda ndipo utafute anayekufaa.

Nikukaribishe siku nyingine kwa mada kazi zaidi zenye mafunzo mengi yanayohusu mapenzi.

Makala hizi zitakuwa zinakujia kila Jumamosi na Jumapili hapa hapa Bongo5.

Kwa mawasiliano zaidi kwaajili ya ishu za mahusiano nicheki kwa namba: +255620744592 ni-SMS au WhatsApp.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW