Habari

Rose Ndauka adai kupumzika kuigiza kwa muda sababu filamu za Bongo zinafanana

Muigizaji wa kike nchini, Rose Ndauka amedai anapumzika kwa mwaka mmoja kufanya filamu kutokana na kijirudia rudia kwa matukio katika filamu nyingi za Kitanzania.

IMG_9680rrr

Akizungumza na Mwanaspoti, Ndauka alisema wazo hilo limetokana na tatizo la kufanya kazi zinazojirudia mara kwa mara, hali iliyomfanya aamue kujipa likizo ya muda ili kujipanga.

“Nimeamua kupumzika kwa kipindi cha mwaka mmoja, sitafanya filamu wala sitakuwa ndani ya tasnia hii. Uamuzi huo nimefanya mwenyewe kwa mawazo yangu na wala sijashawishiwa na mtu yeyote na nimepata msukumo baada ya kuona hakuna kitu kipya ninachofanya,” alisema Ndauka.

“Ninataka nifanye kitu kizuri kwa Watanzania, nasimama kwa muda, lakini nina kazi nyingi ambazo bado hazijatoka hizi nitaziachia kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja, kwani tatizo kubwa kwa wale wanaoona wanauza hawataki kubadilika kila siku wanakuja na kitu kile ile.”

Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuwa na utata muigizaji huyo ni mjamzito kwa sasa na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu kubwa ya yeye kusimama kwa muda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents