Michezo

Kufuatia kipigo cha goli 5-0 cha Simba vs Al Ahly, Haji Manara atoa ahadi hii kwa mashabiki wa Simba

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa, timu hiyo lazima ivune alama 9 katika michezo mitatu ya klabu bingwa barani Afrika, kwenye mechi zote ya nyumbani.

Related image

Manara ametoa kauli hiyo, ikiwa bado mashabiki wa klabu hiyo wanamachungu ya kipigo cha goli 5-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye mchezo uliopigwa jana usiku.

Poleni sana Wanasimba wote, Najua mnavyojisikia now ila niwaambie hesabu zipo kwetu,kama ninavyowaambia always,lazima tupate points tisa za nyumbani!! Yes tukifanikiwa kushinda mechi mbili zilizobaki za home,wanaowacharura leo watawapa hongera!! “ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Jana Simba walinyukwa goli 5-0 dhidi ya waarabu wa Misri, Al Ahly kwenye mchezo wa makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents