Michezo

Kufuatia kipigo cha goli 5-0 cha Simba Vs AS Vita, Haji Manara apoza machungu kwa Yanga SC

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya timu yake kunyukwa goli 5-0 dhidi ya Klabu ya AS Vita ya DR Congo, kwenye mchezo wa klabu Bingwa barani Afrika .

Image result for haji manara vs yanga

Manara licha ya kukiri wazi timu yake kufungwa, kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa kipigo hicho kinamkumbusha miaka ya nyuma wakati Simba walivyowanyuka Yanga goli 5-0 kunako dimba la Taifa.

Nani aliokwambia Simba ndio wa kwanza kufungwa Tano?hebu Gongowazi njooni hapa,lini tuliwafunga tano mara ya mwisho, au mwajitoa fahamu? Na vp kale kananiu nasikia Stand wamekinaniliu? Au bado kipo?,“ameandika Haji Manara .

Kufuatia matokeo ya mchezo huo, Simba inakuwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Kundi D, huku Al Ahly ikiongoza na ikifuatiwa na AS Vita na JS Saoura ikishika mkia.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents