Burudani

Kufungiwa nyimbo za Diamond, Nay kwamuibua Mtangazaji wa E FM, Jabir Saleh (+video)

Mtangazaji wa kipindi cha Ladha 3600 cha E FM, Jabir Saleh amezungumza kuhusu wasanii waliofungiwa nyimbo zao na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kwa kile kilichoelezwa kuwa kinyume na maadili.

Akizungumza na Bongo5 Jabir amesema suala hilo ni lazima lingekuwa na mfumo maalumu wa kushughulika nalo kwa kuangalia wakati wa sasa, pia wasanii na ma-producer watoa nyimbo zenye version tofauti tofauti kulingana na tabaka lengwa.

“Inatakiwa tuangalie tunaelekea wapi na tunataka nini, je nyimbo zinazofungiwa zina matatizo gani na ukilinganisha na mambo yanavyokwenda. Kwa mfano kwa wenzetu albamu inapotoka inaandikwa hii albamu ni version mbili kwa watu aina mbili tofauti hata nyimbo zinapotoka kunakuwa na za radio na nyingine zinaachiwa kwa ajili ya mtaa,” amesema.

“Pia wasanii na ma-producer wanapotoa wimbo wakaona kuna controversy song waangalie kwa sababu kila nchi ina sheria zake, ni muhimu kufuata sheria lakini pia kuwe na version mbili ili kujua anayefuata hii ni mtu mzima,” amesisitiza.

Ameongeza kwa kutolea mfano wimbo wa msanii wa Marekani, Nelly uitwao EI kwa kusema licha ya kufanya vizuri duniania kote muimbaji huyo alitoa version nyingine kwa ajili ya watu wazima na namna ilivyotoka si rahisi kwa yeyote chini ya umri kuipata kwani hata katika mtandao wa YouTube haipatikani.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili na ndio wasanii walifungiwa nyimbo nyingi zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents