Kuishauri Chelsea kufanya usajili ni majanga – Antonio Conte

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amekiri kuwa ni janga kubwa kwa sasa linapokuja swala la kuishawishi timu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wengine.

Conte raia wa Italia amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akikinzana na sera za usajili za timu hiyo hasa wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari na kuonyesha kuwa hana mamlaka ya kusema zaidi nani anapaswa kusajiliwa na klabu hiyo.

Mabingwa hao watetezi wameshuka hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza hii ikitokana na matokeo mabovu ya mfululizo waliyopata dhidi ya Bournemouth na Watford  na kuifanya timu hii kuzidiwa jumla ya pointo 22 na vinara wa ligi hiyo Manchester  City wenye alama 72 wakati wakikabiliwa na mchezo wa ugenini na West Brom usiku wa Jumatatu.

“Hii ndiyo kazi yangu na naifurahia lakini kuna tatizo kuishawishi klabu kununua wachezaji naamini nikifanikiwa katika hilo naweza kufanya vizuri,”meneja huyo wa Chelsea Antonio Conte ameyasema hayo ikiwa timu yake inaelekea kwenye mchezo usiku wa leo dhidi ya West Brom.

“Na paswa kujifunza mengi kutoka kwa kwa makocha wengine ambao hutumia pesa kununua wachezaji.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW