Habari

Kujipodoa Kupita Kiasi!

Kuanzia kwenye ngozi nyeusi hadi kwenye ngozi nyeupe, kupata rangi inayoendena na ngozi yako ni vigumu na ni wazi kutokana na jinsi wasichana wanavyojipodoa, ni vigumu zaidi kwa baadhi ya watu.


Wanawake wengi Watanzania, ambao rangi zao hutofautiana kuanzia rangi zenye weupe wa maji ya kunde wastani hadi weusi zaidi, aghalabu hukosea rangi za vipodozi ama kwa kujipodoa sana au kwa kukosea rangi.

Jambo zuri la kuzingatia wakati wa kupodoa ngozi nyeusi, ni kwamba inahitaji kuongezewa rangi kidogo tu kuonesha sifa zake vizuri, hakuna haja ya kufunika sura yote. Vipodozi vinavyo mfaa mtu mmoja siyo lazima viwafae watu wote.

Msingi au Fondesheni
HAPANA kubwa kwa rangi ya fondeshani ilipauka kuliko rangi ya ngozi, utafafana kinyago na itaonekana feki. Wasichana wengi wanapendelea kujipaka poda kwa mfano “Baby Johnson’s baby powder”, lakini haiendani na ngozi zao, na huchekesha tu. Sababu kuu ya kuweka fondeshani ni kusawazisha ngozi ya usoni, kwa hiyo unahitaji kupata rangi inayopatana na rangi ya ngozi yako.

Unaweza kuchagua kutoka fondesheni za maji, ya poda, isiyo na mafuta, na nimegundua kuwa fondesheni ya poda au unga ni bora zaidi, kwa sababu inaonekana ya kiasilia na hudumu muda mrefu zaidi, lakini hata ya maji hufaa juu ya ngozi nyeusi. Pia hakikisha kuwa kabla ya kupaka fondesheni, ngozi ya uso wako iwe safi, imeoshwa, na kupakwa dawa ya kubana ngozi au toner.

Vipodozi vya Macho
Kwa watu ambao wana rangi iliyokolea zaidi kama maji ya kunde hadi nyeusi zaidi rangi nzuri ya kupaka juu ya macho ni dhahabu, damu ya mzee, hudhurungi na shaba. Ikiwa unapendelea rangi zilizopauka, hakikisha kuwa unapaka sehemu za juu tu karibu na kope kama mstari wa wanja,
Chombo kizuri unachoweza kuwa nacho ni kikunja kope, husaidia kufanya macho yako yaonekane makubwa zaidi, na upakapo mascara huongeza uzuri wa sura yako. Unapo oaka wanja wa maji, ikiwa ni mchana, tumia wanja rangi ya chakleti na usiku wanja mweusi.

Poda ya Mashavu
Ukiwa na rangi iliyokolea sana kuelekea weusi, ni vigumu kupata rangi inayofaa ya poda ya mashavu, lakini unapofanikiwa, kweli utaonekana mzuri sana. Wasichana wengi hukosea rangi na huonekana kama vinyago au mtoto anayejaribu kujipodoa na rangi za mamake mara ya kwanza. Unapaswa kuchagua  rangi za matumbawe, zafarani  iliyokolea na rangi nyekundu, ukitaka kujipaka rangi usiku, ongeza dhahabu kidogo na vimetameta.

Rangi ya Mdomo
Hapa ndipo wasichana wenye rangi iliyokolea sana kuelekea weusi wanapokosea, kwa sababu wanapomaliza kujipodoa wanakuwa wameongeza rangi nyingi hata kuchukiza, haswa wakiwa na midomo mikubwa. Makosa huonekana zaidi. Unachohitaji ni ni kufanya  midomo yako ionekane  mizuri yenye kutamanika, kwa hiyo achana na rangi zilizokolea kama machungwa, HAITAKIWI KABISA. Baadhi ya   rangi, hudhurungi, damu ya mzee, zambarau, matunda damu, krimu, wardi iliyopauka na dhahabu. Rangi nyingine zinazofaa ni kahawia, chakleti, damu ya mzee  iliyokolea, mvinyo, wardi na maziwa hupendeza juu ya ngozi nyeusi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents