Habari

Kukata jongoo kwa meno kuna hitaji ujasiri – Dkt. Kikwete

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa miaka miwili kimefanikiwa vizuri huku akisema kuwa mwaka 2020 lazima warudi kwa wananchi na kama hawajayatimiza yale waliyowaahidi watakwenda kuwaambia nini wananchi.

Dkt. Kikwete Rais amesema hayo leo katika Mkutano Mkuu wa 9 wa CCM unaoendelea mjini Dodoma ambapo pamoja na hayo ili kuwa ili uweze kufanikiwa inahitaji ujasiri kama msemo wa Kiswahili unaosema una mkata jongoo kwa meno maana kukata jongoo kwa meno kuna hitaji ujasiri.

“Katika miaka miwili hii kwanza mipango walioipanga wamekwisha ifanya, ilani kwanza na mipango waliyoibuni wenyewe ndani ya serikali ni mizuri sana, kuhusu ilani niseme tu tumepata watu, viongozi ambao ni wasimamizi wazuri sana wa ilani ya Chama cha Mapinduzi watekelezaji hodari ni watu makini, watu wabunifu na ni watu jasiri maana mengine anayoyafanya yanahitaji ujasiri na ule msemo wa Kiswahili unaosema unakata jongoo kwa meno, kukata jongoo kwa meno kuna hitaji ujasiri lakini ndio sifa ya kufanikiwa ndani ya miaka miwili hii tumefanikiwa vizuri na mipango tuliyokuwa nayo inaleta matumaini, inaleta matumaini kwa taifa, imeleta matumaini kwa taifa na Chama cha Mapinduzi,” amesema Dkt. Kikwete.

“Hatimae mwaka 2020 lazima turudi kwa wananchi tutakwenda kuwaambia nini yote yale ambayo tuliyaahidi kuyafanya yale ya ziada ambaypo viongozi hawa walikaa ndani ya serikali kutafakari hali ilivyo na ilani ile tulitengeneza sisi kwa uthabiti watakapo ingia wao watakaa chini wataitazama ilani wanatengeneza mipango yao na namna ya kutengeneza mikakati ya kutengeneza ile ilani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents