BurudaniHabari

Kukurupuka kutaua Bongo Flava

Msanii mkali wa miondoko ya RnB nchini..Banana Ali Zorro, amesema hivi karibuni alikua akifanya utafiti wa kujua kinachosababisha kutodumu kwenye chati kwa muda mrefu kwa nyimbo za Bongo Flava.

Akiongea mwishoni mwa wiki Banana alisema utafiti huo umemfanya abaini sababu za maisha mafupi ya nyimbo hizi za Bongo Flava…ambapo alisema kunasababishwa na kukurupuka tu kwa wasanii kutoa nyimbo kila kukicha na kujali zaidi maslahi yao kuliko kile wanachowalisha mashabiki wao.

Akiendelea anasema…ā€¯ukijali zaidi maslahi ..utajikuta unaadaa wimbo mmoja tu wa kibiashara (utakaohit)…lakini pia utakaokua hauna msessage yoyote ya maana..then unatengeneza na track zingine kadhaa unakua ushamaliza albam unaiingiza sokoni!!!…hivi kweli albam ya aina hii inaweza kudumu kwenye chati kwa muda mrefu kweli?..anauliza msanii huyu.

Akitetea hoja yako hiyo..msanii huyo alisema kutokana na umakini anaoutumia kutengeneza songi zake…ndio maana ameweza kukaa miaka minne kabla ya kutoka na albam nyingine itakayoingia mtaani wakati wowote.

Akimalizia msanii huyo alisema….mimi bwana natoka kama Michael Jackson,albam moja kila baada ya miaka minne hahaha. A

lbam ya kwanza ya msanii huyo iliyoitwa (Banana) ilitoka mwaka 2002.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents