Michezo

Kumbakiza David de Gea ndiyo kibarua kikubwa kilichopo ndani ya Manchester United kwa sasa 

Baada ya misukosuko ya hapa na pale inayopitia klabu ya Manchester United hasa katika upande wa kocha wake Mourinho, Paul Pogba na hata kushindwa kufanya vizuri kwenye baadhi ya mechi zake, timu hiyo kwa sasa inakabiliwa na kibarua kikubwa wa kuhakikisha inambakiza mlindalango namba moja David de Gea katika dirisha lijalo la usajili.

Kwenye mahojiano maalumu na Sky Sport, De Gea amenukuliwa akisema kuwa kwa sasa mawazo yake yapo katika kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mechi zao zijazo na siyo kufikiria mkataba na Manchester United.

Meneja wa United, Jose Mourinho Ijumaa hii amesikika akisema kuwa hana uhakika kama watafanikiwa kuongeza mkataba na goli kipa huyo raia wa Hispania lakini mazungumzo bado yanaendelea.

Wakati Manchester United ikielekea kwenye mchezo wake dhidi ya Everton Jumapili hii, De Gea amesema kuwa anaepukana na mazungumzo yoyote yatakayousiana mkataba wake mpya.

“Kitu muhimu ni timu na sote tumehamishia mawazo yetu yote tumehamishia huko, ambapo tunahitaji kushinda, ni kitu muhimu zaidi kuliko maswala ya mikataba,” amesema De Gea.

“Tuna mchezo muhimu dhidi ya Everton na tunaratiba kubwa mwezi ujao nafikiri hicho ndiyo kitu muhimu kuliko kuwazia jambo lingine lolote.”

“Nimekuwa hapa kwa mismu mingi tu, nimekuwa ndani ya klabu kwa misimu nane sasa. Najiskia furaha kuwa hapa.”

Kiwango cha Man United msimu huu na maswala ya Mourinho yamekuwa yakijadiliwa kila mahala wiki za hivi karibuni lakini pia klabu hiyo ikiwa kwenye nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kwakupoteza michezo yake mitatu imekuwa moja kati ya mada kubwa kwenye vyombo vya habari na mashabiki kwa ujumla.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents