Shinda na SIM Account

Kumbe hawa ndio wabrazil waliompeleka Philippe Coutinho Barcelona!

Jina la Philippe Coutinho ndio linazungumzwa sana kwa sasa katika tasnia ya soka kutokana na usajili wake kutoka Liverpool kwenda Barcelona kuzua taharuki kubwa.

Mchezaji huyo amesajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 145 ambapo usajili wake huo umeweza kuweka rekodi kwa vinara hao wa La Liga kwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa fedha nyingi zaidi akifuatiwa na Ousmane Dembélé aliyesajiliwa kwa paundi milioni 105 akitokea Borussia Dortmund.

Coutinho ambaye Jumatatu hii alitangazwa mbele ya waandishi wa habari katika uwanja wa Camp Nou anakuwa mchezaji wa 33 kutoka taifa la Brazil kusajiliwa na Barca.

Hawa ni wachezaji wengine kutoka nchi hiyo ambao wamewahi kusajiliwa na kuchezea Barcelona.

1.Fausto Dos Santos (1931-32)
2.Jaguare (1931-32)
3.Lucidio Batista (1947-49)
4.Evaristo De Macedo (1957-62)
5.Walter Machado (1966-67)
6.Marinho Peres (1974-76)
7.Bio (1977-79)
8.Roberto Dinamite (1980)
9.Cleo (1982)
10.Aloisio Pires (1988-90)
11.Romario (1993-95)
12.Giovanni (1996-99)
13.Ronaldo (1996-97)
14.Sonny Anderson (1997-99)
15.Rivaldo (1997-2002)
16.Thiago Motta (2001-07)
17.Fabio Rochemback (2001-03)
18.Geovanni (2002-03)
19.Ronaldinho (2003-08)
20.Juliano Belletti (2004-07)
21.Sylvinho (2004-09)
22.Edmilson (2004-08)
23.Henrique (2008-12)
24.Keirrison (2009)
25.Dani Alves (2008-16)
26.Maxwell (2009-12)
27.Adriano Correia (2010-16)
28.Neymar (2013-17)
29.Rafinha (2013-present)
30.Douglas (2014-present)
31.Marlon (2017-present)
32.Paulinho (2017-present)

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW