Burudani

Kumbe ishu sio Tuzo: Monalisa afunguka ‘bifu’ la Wema na Riyama

Baada ya kumalizika drama za hapa na pale kati ya Wema Sepetu na Rihama Ally, msanii wa Filamu Bongo, Monalisa amesema malalamiko ya Riyama yalikuwa ni zaidi ya tuzo aliyoshinda Wema.

Awali Rihaya alikuwa akilalamika kuhusu kushindanishwa na Wema Sepetu katika tuzo za za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) na Wema kushinda tuzo hiyo.

Hata hivyo wawili hao walionekana kupatana mara baada ya kukutana katika kumpokea Monalisa akitokea Nigeria ambapo alishinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika..

“Kwanza niseme nilivyofika pale sikutegemea kuona watu lakini nilivyoshuka nikakutana na wasanii wenzangu, nilijisikia furaha sana,” amesema Monalisa.

“Nilifurahi kuawaona, sidhani kama Riyama kamlalamikia Wema nyie tu ndio mnachukulia vibaya, Riyama alikuwa na malalamiko yake na mimi ninayafahamu toka siku ya kwanza,” Monalisa ameiambia Times FM.

Ameongeza kuwa Riyama na Wema wote ni rafiki zake na anaongea nao vizuri na wote si watu wa vinyongo.

April Mosi mwaka huu Wema Sepetu aliibuka mshindi wa tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF),

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents