Burudani

Kumbe wimbo mpya wa Beyonce ‘Grown Woman’ ulivuja

Jana tuliweka wimbo mpya wa pop/R&B diva Beyonce ‘Grown Woman’ ambao taarifa zilizopatikana inasemekana kuwa wimbo huo ulivuja mtandaoni.

beyonce-knowles-06

Kuvuja kwa ‘Grown Woman’ kulichangiwa na kusambaa kwa kipande cha wimbo huo kilichotumika katika tangazo la biashara la Pepsi, na pia Beyonce aliuimba live katika moja ya show zake ya Mrs Carter World tour huko Paris mwezi uliopita.

Wimbo wa “Grown Woman” ambao umetengenezwa na producer mkongwe Timberland utakuwepo katika album ya 4 ya Bey ambayo mpaka sasa haijajulikana itaitwaje na itatoka lini.

Sikiliza jinsi mashabiki wenye kiu ya wimbo huu mkali walivyounganisha kipande kilichotumika katika tangazo na kuufanya kuwa wimbo kamili. Track ni kali, inachezeka na tunaamini itafanya vizuri.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/90059348″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents