Makala

Kumbukumbu: Mashabiki wa Man United wanavyotokwa machozi wanapo mkumbuka Rooney wa Ferguson

Siku ya leo inaweza ikawa ni kumbukumbu nzuri au mbaya zaidi kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United, hasa wanapoukumbuka usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wao Wayne Rooney aliyejiunga na Everton.

Mashambuliaji huyo atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa ndani ya United na kufanikiwa kuweka rekodi ya kuwa mfungaji boa wa muda wote ndani ya timu hiyo kwa kufunga mabao 250 na kuipiku rekodi ya Bobby Charlton iliyodumu kwa muda mrefu.

Chini ya utawala wa kocha Sir Alex Ferguson wa miaka takribani 13 iliyopita, ulifanikiwa kuinasa saini ya Rooney ambaye alikuwa akiichezea Everton kwa wakati huo na alikuwa ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 19 kasoro.

Rooney alisajiiwa kwa kiasi cha paundi milioni 25.6 na kuwa mchezaji mwenye umri chini ya miaka 20 ambaye amesajiliwa kwa fedha nyingi zaidi. Wakati huo huo Everton ilikuwa imeweza kukataa ofa kutoka kwa Newcastle ya kumsajili mchezaji huyo kwa paundi milioni 20.

Rooney alikabidhiwa jezi namba nane kwa mara ya kwanza ndani ya Manchester na alionekana ni mchezaji ambaye alikuwa akiiota kila siku nafasi hiyo aliyoipata. “I’m excited to be joining a club as big as Manchester United. I feel this can only improve my career,” haya ndio maneno aliyozungumza mshambuliaji huyo baada ya kusaini United.

Mshambuliaji huyo alianza kuonyesha thamani yake Septemba 28 ya mwaka huo 2004 katika mchezo wa UEFA kwa kufunga hat trick yake ya kwanza akiwa na Man United katika ushindi wa mabao 6–2 dhidi ya Fenerbahçe.

Goli la mwisho la Rooney kuifungia United lilikuwa dhidi ya Stoke City katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika Januari 21 ya mwaka huu katika uwanja wa bet365 ambapo lilikuwa lakusawazisha na kumfanya mchezaji huyo afikishe mabao 250 na kuwa mfungaji kinara wa muda wote katika klabu ya Manchester United.

Hatimaye Julai 9 ya mwaka huu Rooney alirejea katika klabu yake ya Everton baada ya kupita kwa miaka 13. Wacha mashabiki wa Manchester United walie wanapoikumbuka miguu ya Rooney na magoli yake yalivyokuwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents