Habari

Kumeza dawa kwa kutumia maji ya baridi ni hatari kwa afya yako? Huu ndio ukweli

Unaweza ukatumia maji ya baridi kumezea dawa zako. Pindi umezapo dawa kwa kutumia maji ya baridi, mwili umejitengenezea namna ambayo huanza kuyapasha maji hayo joto pindi yatakapofika tumboni.

Mchanganyiko huo wa maji na dawa hukaa kwenye tumbo kwa muda wa dakika 20 (kama chakula na vinywaji vingine). Kwahiyo ndani ya dakika 5 maji yameshapashwa joto na kufikia jito la kwenye tumbo (stomach temperature), hakuna madhara yeyote unayoweza kupata ya kiafya. Mwili huweza kuvumilia kiasi kikubwa cha utofauti wa hali mbalimbali.

Mwili hutumia nguvu ili kuweza kupasha joto maji, kwahiyo ni vizuri kutumia maji ambayo yamepoa kumezea dawa zako ili kuupunguzia mwili kazi ya kuyapasha joto maji kama yatakua ya baridi, maana dawa huhutaji joto mwili fulani ili kuweza kumeng’enya na kuifanya dawa ipenye kwenye kuta za tumbo kirahisi kuingia kwenye damu.

Lakini niwatoe hofu kuwa hakuna madhara yeyote ya kiafya unayoweza kuyapata kwa kumeza dawa kwa kutumia maji ya baridi.

Your Health, Our Concern

FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/Pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents