Kumuona 50 Cent ni elfu 50 kwa 30

Kampuni ya simu za mkononi Tigo imetangaza rasmi kiingilio katika onesho la msanii kutoka Marekani 50 Cent, ambapo cha juu kitakuwa ni sh. 50,000 wakati cha chini ni sh. 30,000

50 Cent


 


Kampuni ya simu za mkononi Tigo imetangaza rasmi kiingilio katika onesho la msanii kutoka Marekani 50 Cent, ambapo cha juu kitakuwa ni sh. 50,000 wakati cha chini ni sh. 30,000.


 


Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Kelvin Twissa alisema wameamua kuweka kiingilio hicho, ili kila Mtanzania apate nafasi ya kumuona mwanamuziki huyo katika onesho atakalolifanya ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Mei 4, mwaka huu.


 


Alisema mbali na mashabiki kulipia kiasi hicho pia watatoa tiketi 700 bure kwa wateja wazuri wa mtandao huo, ambapo watalazimika kutuma neno muziki kwenda kwenye namba 15315 na kujishindia tiketi za bure.


 


Alisema sh. 50,000 itakuwa viti maalum, wakati sh. 30,000 itakuwa viti vya kawaida na kuongeza kuwa wana imani mashabiki watafurahia onesho hilo.
Kazi kwenu wabongo mtu mzima ndio huyo anadrop.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents