Habari

Kuna baadhi ya Wabunge waliingia mitini kupima VVU – Spika Ndugai (+video)

Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewakumbusha wabunge kupeleka habari ya kupima Virusi vya Ukimwi kama walvyopima baadhi ya wabunge huku akisema kuna baadhi waliingia mitini (hawakupima).

Ndugai ameyasema hayo leo baada ya Waziri mjuu, kassim majaliwa kuwasilisha hoja ya kuharisha bunge la Bajeti lililokuwa likiendelea Jijini Dodoma.

“Mh. waziri Mkuu ametukumbusha habari ya kupima VVU, yeye alipima na mimi nikamuunga mkono nikapimwa na wengine baadhi mkafanya hivyo lakini baadhi waliingia mitini kupima. Ombi letu ni kwamba tunapoenda Majimboni iwe ni moja ya agenda zetu ambazo tutazifikisha kwa wananchi wetu,”amesema Spika Ndugai.

Bunge limehairishwa rasmi leo,Juni 29,2018 hadi tarehe 4 Septemba, 2018 Siku ya Jumanne) saa 3 kamili asubuhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents