Burudani

Kuna kitu gani kinaendelea kati ya Harmonize na uongozi wa WCB?

Mwanzoni mwa mwaka huu February 6, 2019 muimbaji, Harmonize alitangaza kuachia EP yake ‘Afro Bongo’ kupitia tukio la kutoa misaada kwa walemavu alililofanyika Mbagala jijini Dar es salaam.

Lakini kwa bahati mbaya alisitisha zoezi hilo baada ya kuitikia wito wa kuripoti Polisi Central kuhojiwa kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi kama RC Makonda alivyoagiza.

Baada ya tukio hilo, muimbaji huyo alitoa taarifa nyingine ya kwamba EP hiyo ataiachia February 18 siku ya jana lakini ilipigwa ‘stop’ tena na uongozi wa WCB na kuahidi siku ya leo watatoa taarifa rasmi.

Jumatano hii mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Sallam SK ametoa taarifa ambayo inaonyesha kuna kitu kinaendelea kati ya uongozi wake na Harmonize.

TAARIFA KWA UMMA.. Maelezo ya utokaji wa EP ya Harmonize @harmonize_tz : Uongozi wa WCB unaomba msamaha kwa ucheleweshaji kama ahadi ya awali ilivyo, muda mwingine msanii anakuwa na shauku kubwa kuwapa mashabiki wake burudani na kufikia sehemu anasahau kuwa hizo burudani pia ni biashara ambayo itakayompatia kipato yeye ili aweze kutoa burudani zingine, kama uongozi lazima tumuandalie misingi ya kibiashara ili anufaike na kazi zake pia, na vilevile tusiwe na matabaka ya kuwajali mashabiki wa sehemu moja pale kazi zinapotoka, inatakiwa kama uongozi kuhakikisha kazi ya msanii inapatikana sehemu zote kukidhi hamu za mashabiki wote, kingine unapofanya kazi na wasanii waliopo lebo kubwa inahitajika lebo zao waweze kutia saini mikataba ya mirabaha ili nyimbo ziweze kuwepo kwenye mitandao yote ya mauzo ili isilete matatizo kwenye lebo zao. Kwahiyo ukubwa wa EP ya Harmonize ilihitaji kupitia yote hayo ili iwe tayari kufika kwa mashabiki, tunashukuru Basata walitoa ushirikiano mzuri kuzikagua nyimbo kwa muda muafaka na hakutokua na tatizo la wimbo unatoka halafu unafungiwa. Kwa haya mafupi sasa EP ya Harmonize ya #AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi. Tunaomba radhi kwa yoyote tuliyemkwaza kwa namna moja ama nyingine tunajua bila nyie mashabiki hakuna WCB. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI BONGO FLAVA 🙏🏽

Taarifa hii inaibua maswali mengi juu ya mahusiano kati ya WCB na muimbaji huyo wa Kwangwaru

.Uongozi wa WCB haukutangaza kwamba Harmonize ataachia EP

Waswahili wana usemi usemao ‘Mwiba hutokea pale ulipoingia’. Kama Harmonize mwenyewe angetangaza kama nasitisha kuachia EP yake kutokana na sababu za kibiashara isingekuwa big ishu. Lakini mpaka WCB wanaingilia na kusitisha kutoka kwa EP hiyo inamaanisha kwamba hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya Harmonize na uongozi wa WCB.

  Harmonize amejitengenezea ‘Empire’ yake ndani ya WCB.

Hakuna anayebisha kwamba kwa sasa Harmonize ni mkubwa sana kwa wasanii WCB ukimtoa Diamond. Tena sio mkubwa tu kimuziki bali hata kwa kipato hata rais wa label hiyo, Diamond alithitisha hilo.

Katika mazingira hayo huwenda pia kuna baadhi ya watu anawasikiliza zaidi na kuwashirisha baadhi ya mambo yake ndio maana kumekuwa kukitokea sitomfahamu kama ya ishu ya kutoka EP.

EP ya Harmonize ya AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi.

Kwa mujibu wa sentensi hii (hapo juu) iliyotolewa na Sallam inaonekana kuna kitu kinaendelea, kwani hiyo EP ya AfroBongo ilikuwa inatoka chini ya label gani?. Kauli kama hizi zinaacha maswali mengi kwa mashabiki wengi wa muziki namna Harmonize anavyoweza kutangaza jambo akiwa ndani ya kampuni bila mabosi wake kujua.

Mashabiki waushitukia mchezo

Baada ya vitu hivyo kutokea tayari kuna baadhi ya mashabiki wanatafsiri huwenda kukawa na tatizo kati ya Harmonize na uongozi wake. Soma maoni hapo chini.

Mahmoudahamad28 “Mnazingua mnasema itatoka week ijayo chini ya#wcb kwani b4 ilikuwa itoke chini ya nani??”

Charlz_rick @sallam_sk nahisi haya yote yalitakiwa kuangiliwa na uongozi mzima wa WCB kabla ya kutangaza tarehe kwa sabbu hii ni mara ya pili kuahirishwa”

Sumalito “Kwani kabla ilikua itoke chini ya lebel gani? harmonise c yupo wcb au saivi ana lebel yake. l.,”

Kibokilo “Ambao tumejaribu kumuelewa boss na kuchukizwa na kiherehere cha harmonize tugonge like hapa,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents