Habari

Video: Kuna watu wananichongamisha na viongozi wangu – RC Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amesema kuna gazeti moja nchini limekuwa likiandika habari za kumchonganisha yeye na viongozi wengine au taasisi nyingine za serikali, jambo ambalo amesema halikubaliki wala hawezi kulifumbia macho.

Makonda ameyasema hayo leo, Feb. 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa Jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Amana, iliyopo Ilala jijini Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kauli hiyo ya Makonda imekuja kutokana na maamuzi yake ya kuvunja mabaraza yote ya ardhi ya mkoa wa Dar, na kutaka kazi hizo zifanywe na makatibu tarafa hadi pale ambapo utaratibu mwingine utawekwa, jambo ambalo baadhi ya vyombo vya habari na wanaharakati walidai kuwa anaingilia kazi ya mahakama.

“Kuna gazeti moja linahangaika sana kuandika vitu vibaya kuhusu Mkoa wa Dar, wanajifanya wanajua sana sheria, wanachonganisha, na leo nimeona wameandika tena, wasitupotezee muda.

“Aliyeanza kugombanisha duniani ni shetani, lakini ilifika wakati akashindwa, hili gazeti raha yao wanataka wasikie mahakama imemkataa Mkuu wa Mkoa, hawaoni mateso ya wanachi wala kuyaripoti.

“Sasa aelewe tu kwamba hawatafanikiwa, nimeangalia nikabaini kuna ardhi moja bosi wao aliichukuaga, ipo tu limebaki poli katika eneo moja katika Wilaya ya Ubungo, tutaangalia taratibu angalau tuwapatie watu lijengwe soko la kisasa pale,” alisema Makonda bila kutaja ni gazeti gani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents