Tupo Nawe

Kundi jipya la wasanii watano F Starz kujitambulisha soon

Kundi jipya la muziki wa Bongo Flava, la F Staz ambalo ni muunganiko wa wasanii watano , Y TONY, MIRROR,SHADOOH,PAPAA MASAI,NA NUH ambao wanasimamiwa na mameneja tofauti tofauti akiwemo ni shabaha,hk,mr kapongo,bad, na muro wanatarajiwa kufanya shoo ya nguvu tamasha kubwa la kujitambulisha siku ya tarehe 7 mwezi wanne katika ukumbi wa Club Maisha jijini Dar-es-Salaam.

F Straz Emage 1 (1) (500x352)

Vijana hao wachanga lakini wenye vipaji vya hali ya juu katika bongo flava, wanatarajiwa kuwika na kuwa wasanii wakubwa kama watafanikiwa kubakia pamoja kwa muda mrefu bila kusambaratika.

Baada ya shoo yao ya utambulisho pale Maisha wasanii hao wa F Stars watazunguka katika maeneo tofauti tofauti katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao.

Msanii Shadoo anatamba na wimbo wake wa “By show”, wakati msanii Papaa Masai anatamba na wimbo wa “Ng’ari ng’ari” aliomshirikisha Ali Kiba, wakati msanii Miro akitamba na wimbo wake wa mapenzi “Si kama zamani” huku msanii Y tony naye akitamba na kibao chake cha “Sijazoea masebene”.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW