Burudani

Kundi la Chris Brown wazichapa na Migos kwenye BET (Video)

Chris Brown anaonekana bado anahasira na kundi la muziki la Migos hasa Quavo ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na ex wake Karrueche Tran.

Muimbaji huyo aliyetumbuiza katika utoaji wa tuzo za BET wikiendi hii na baada ya kumalizika kwa sherehe ya tuzo hizo na kuhamia katika After Party, alijikuta kundo lake likianza ugomvi kwa kutupiana makonde na Migos.

Mmoja ya watu walioshuhudia tukio hilo, ameuambia mtandao wa TMZ, kundi la Chris ndio walianzisha ugomvi huo kwa kumpiga mmoja wa member wa kundi la Migos kwa makusudi. “Kundi la Chris ndiyo walianza ugomvi huo kwa kumpiga mtu kutoka kwa Migos, ambapo walimpiga mtu huyo kwa makusudi.”

“Chris alikuwa yupo karibu na Future na Dj Khaled pamoja na familia yake baada ya ugomvi kuwa mkubwa. Mtoto wa Khaled [Asahd] alianza kulia, hata hivyo Chris hakuonekana kurusha ngumi na mpaka tunatoka ugomvi uliamia sehemu ya parking na hakuna aliyekamatwa,” ameongeza shahidi huyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents