DStv Inogilee!

Kundi la Jambo Show kutoka Tanzania lafanya maangamizi kwenye usaili wa shindano la Israel’s Got Talent (+video)

Kundi la Jambo Show kutoka Tanzania lenye maskani yake nchini Israel limeonesha matumaini ya kufanya vizuri kwenye msimu mpya wa Israel’s Got Talent, baada ya kufanya vizuri kwenye usaili wa kufuzu kuingia hatua ya makundi.

Kundi la Jambo Show linaloundwa na wasanii watano, lilitumbuiza kwa takribani dakika 3 jukwaani. Tukio ambalo liliwanyanyua majaji wa shindano hilo na kuanza kuwapigia makofi vijana hao.

Shindano la Israel’s Got Talent msimu wa pili, limeanza wiki iliyopita na linatarajiwa kumalizika mwezi Februari mwakani, na unaweza kuangalia moja kwa moja kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za kituo cha runinga cha Rashet TV.

Hata hivyo, ukawapigia kura Jambo Show ili waweze kufanikiwa kufuzu kwenye shindano hilo kwa kubofya link ifuatayo https://reshet.tv/item/vod/got-talent/season-02/clips/jumbo_show-941334/

 

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW