Habari

Kundi la kwanza la raia wa Nigeria wakiwa 188 lawasili jijini Lagos kutoka Afrika Kusini

Kundi la kwanza la raia wa Nigeria wakiwa 188 lawasili jijini Lagos kutoka Afrika Kusini

Kundi la kwanza la raia wa Nigeria wamekimbia vurugu zinatotokana na chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini limewasili mjini Lagos. Watu 188 waliokuwa ndani ya ndege wakitoka Johannesburg ni wa kwanza kurejea miongoni mwa takriban raia 600 wa Nigeria ambao walikuwa tayari kurejea nyumbani baada ya kutokea vurugu ambazo zililenga biashara za raia wa kigeni.

Mmoja kati ya waliorejea, Israel Oluwaseun, k”Nimekutana na mazingira ya vurugu za chuki nchini Afrika Kusini. Nilishawahi kukumbana na hali hiyo mwaka 2014, nilikutana na tukio jingine ambalo halikuwa baya sana, lakini ukiitazama, inakua.

”Si jambo ambalo limerekebishwa.” lakini amesema muda wake nchini Afrika Kusini haukupotea bure:

”Sijuti kuwa Afrika Kusini. Ilikuwa funzo kubwa kwangu…imenifanya kuwa na bidii sana katika kufanya kazi. Kufanya kazi kwa bidi na kufikia malengo niliyojiwekea.”

Gazeti la Punch limekuwa likionesha video za raia wa Nigeria wakirejea nyumbani.

Kwa mujibu wa BBC. Mwanaume mmoja abaye alikuwa fundi magari nchini Afrika Kusini, amesema watu waliingia kwenye karakana yake na kuchoma moto eneo lote na kuyachoma magari yote”.

Watu 12 walipoteza maisha kwenye vurumai hizo, lakini kwa mujibu wa serikali ya Afrika Kusini, 10 kati yao ni raia wa Afrika Kusini na hata wengine wawili si raia wa Nigeria.

Raisi wa Nigeria Muhammadu Buhari amepeleka ujumbe wake nchini Afrika Kusini kwa ajili ya ”kueleza masikitiko yao kuhusu namna wanavyotendewa raia wake”.

Katika taarifa, ofisi ya raisi imeiomba Afrika kusini kuchukua hatua kukomesha vitendo vya chuki dhidi ya raia wa kigeni kutoka mataifa mengine ya kiafrika”.

Kadiri majuma yanavyosonga watu wamekuwa wakitumiana video kwa WhatsApp kuonesha vitendo vya mashamulizi dhidi ya raia wa Nigeria.Lakini video hizo zimekuwa zikidaiwa kupotosha watu.

Raia wa Nigeria 640 walisajiliwa katika ubalozi wa Nigeria nchini Afrika Kusini baada ya kutokea mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Nigeria kwenye ukurasa wake wa twitter inakadiriwa kuwa idadi ya raia 313 watachukuliwa kutoka Afrika Kusini katika awamu ya kwanza na waliosalia watasafirishwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents