Burudani

Kundi la Mafikizolo kuvunjika? Huu ndio ukweli

Muimbaji wa kiume wa kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini, Theo Kgosinkwe ameamua kuzielezea tetesi kuwa kundi hilo lipo mbioni kuvunjika.

DSC_0007a_pp.jpg
Nhlanhla Nciza na Theo Kgosinkwe wanaounda kundi la Mafikizolo

Tetesi hizo zilianza baada ya muimbaji wa kike wa kundi hilo, Nhlanhla Nciza kuanzisha kampuni yake fashion na Theo kudai kuwa anaanzisha lebo yake mwenyewe.

“Siondoki na hatuvunjiki kama kundi. Siku zote nimekuwa na ndoto ya kuwa producer na nataka kukuza pia vipaji vichanga. Nahisi kuwa huu ndio muda wa mimi kuanza safari mpya kama producer na mfanyabiashara,” Theo aliliambia jarida la Move!

Tayari Theo ameshamsainisha msanii wa kwanza wa kike aitwaye, Melo kwenye lebo yake, 350 Degrees Entertainment.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents