Burudani

Kundi la One Direction huingiza shilingi milioni 62 kila siku

Kundi maarufu la Uingereza la One Direction, huingiza pauni 19,000 kila siku ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 62.

one-direction-bbma-photo-studio-2015-billboard-650

Waimbaji hao waliopata mafanikio baada ya kuwa chini ya usimamizi wa Simon Cowell kupitia kipindi cha The X Factor mwaka 2010, huingiza kiasi hicho cha fedha kufuatia taarifa zao za fedha zilizochapishwa na Companies House.

One Direction walitengeneza faida ya jumla ya £35m na kampuni yao 1D Media mwaka jana ingawa mwenzao Zayn Malik alijiondoa na kuwaacha Harry Styles, Liam Payne, Niall Horan na Louis Tomlinson.

Pamoja na mafanikio hayo, vijana hao wameamua kupumzika mwakani baada ya kuachia album tano na kufanya ziara nne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents