Habari

Kundi la TLC laikwaza familia ya marehemu ‘Left Eye’ kwa kutoa version mpya ya wimbo wao ‘Waterfalls’ bila sauti yake (Audio)

Familia ya aliyekuwa member wa kundi la kinadada watatu wa TLC marehemu Lisa Nicole Lopes ‘Left Eye’ imekasirishwa na kitendo cha members wawili waliobaki T-Boz na Chili, kufanya version mpya ya hit song yao ya maika ya 90 ‘Waterfalls’ na kuiondoa sauti ya Left Eye bila kuwapa taarifa.

TLC

T-Boz na Chili hivi karibuni wametoa version mpya ya hit song yao ya miaka ya 90 ‘Waterfalls’ kama sehemu ya kuadhimisha 20th annivessary ya kundi hilo.

Kitu ambacho kimeongeza pilipili katika kidonda cha wana ndugu wa mwenzao marehemu Left Eye ni uamuzi wa kuondoa sauti yake katika version mpya ya wimbo huo na kumuweka mwimbaji Namie Amuro wa Japan.

NamieAmuro
Namie Amuro

Akiongea na TMZ dada wa Left Eye aitwaye Reigndrop Lopes amesema hakuwa na taarifa kuhusiana na wimbo huo mpaka shabiki mmoja alipouweka kwenye mtandao, na kuongeza kuwa angalau kama wanafamilia wangepewa japo taarifa kuliko kukutana na wimbo kama surprise katika mtandao. “I did not know about it until a fan posted it online. I mean it would have been nice if they would have given us a head up before being surprised.”

Reigndrop aliongeza kuwa mama yao alishtushwa sana na kuumizwa na kitendo hicho na kusema wangeiacha sauti ya Lisa ingekuwa ni heshima na kumuenzi pia.

Original version ya ‘Waterfalls’ ilikuwa inapatikana katika album ya pili ya TLC ‘Crazy Sexy Cool’ na iliwawezesha kupata tuzo mbili za grammy (1996).

Katika msiba wa Left Eye baadhi ya mistari ya verse yake ya Water falls – “Dreams are hopeless aspirations, in hopes of coming true, believe in yourself, the rest is up to me and you”- yaliandikwa katika jeneza lake kama moja ya mchango wake mkubwa katika hit song hiyo.

Waterfalls (original) iliandikwa na Marqueze Etheridge pamoja na Left Eye (huenda ndio maana familia yake imewauma sana).

Isikilize hapa verion mpya ya ‘Waterfalls’ ya TLC bila sauti ya Lisa ‘Left Eye’ ambaye sehemu yake imeimbwa na Namie Amuro

http://youtu.be/tjMzPh0d5Ic

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents