Burudani

Kundi la Uhuru la Afrika Kusini ladaiwa kuwa kwenye hatihati ya kuvunjika

Kumekuwepo na taarifa kuwa kundi maarufu la Uhuru la Afrika Kusini linaloundwa na Maphorisa, Mapiano, DJ Clap na Xeli,linadaiwa kuwa kwenye hatihati ya kuvunjika.

Uhuru
Members wa kundi la UHURU

Kwa mujibu wa gazeti la Sunday World la Afrika Kusini, inasemekana kuna kutoelewana kati ya member wa kundi hilo Maphorisa ambaye pia ni producer pamoja na members wenzake kiasi cha kuwatenganisha kwenye baadhi ya kazi wanazotakiwa kufanya pamoja.

Miongoni mwa vitu vinavyoonesha dalili hizo, ni kutoonekana kwa members watatu wa undi hilo kwenye video mpya ya Davido ‘The Sound’, ambayo kaonekana Maphorisa peke yake huku walishirikishwa wote kwenye wimbo.

Dalili nyingine inayoashiria matatizo kwenye kundi hilo, ni baada ya Maphorisa kutoonekana kwenye performance ya kundi la Uhuru wakati wa tuzo za Glo-Caf Awards nchini Nigeria. Inadaiwa kuwa meneja wa Maphorisa alilazimika kupanda jukwaani kuziba nafasi yake.

Vyanzo vimeliambia gazeti hilo kuwa Maphorisa kwa sasa hazungumzi na member mwenzake Xeli, na inadaiwa kuwa Maphorisa anajiona ni mkubwa kuliko kundi na amekuwa busy akifanya collabo na wasanii mbalimbali wa Afrika.

“There’s been a rift between them because Maphorisa thinks he’s bigger than the group. Maphorisa is so busy with collaborations and producing with other African artists.”

Maphorisa ndiye producer aliyetengeneza nyimbo mpya za Chege na Temba – Kaunyaka, Madee – Vuvula pamoja na ile ya Linah – Ole Themba iliyotoka mwaka jana.

Source: The Juice / MTV Base

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents