Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Kunenepa kupita kiasi kwa mponza Carlos Tevez China

Kocha mpya wa klabu tajiri nchini China ya Shanghai Shenhua, Wu Jingui ameamua kumtolea uvivu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Carlos Tevez kuwa hawezi kuichezea timu hiyo endapo hatopunguza unene aliyokuwa nao.

Meneja huyo mpya wa Shanghai Shenhua , Wualiyerithi mikoba ya Gus Poyet aliyejiudhuru mapema mwezi huu ameanza kwa kumcharukia mchezaji huyo pamoja na mwenzake Fredy Guarin kwa kuwa na uzani mkubwa.

Meneja , Wu amesema kuwa anawajibika katika kikosi hicho hivyo Tevez na Guarin watalazimika kupunguza uzito ili kuweza kupata namba ndani ya kikosi chake kwakuwa wanashindwa kuwajibika kwa asilimia miamoja wawapo uwanjani.

Carlos Tevez mwenye umri wa miaka 33, ni miongoni mwa wachezaji wanaovuta fedha nyingi duniani  mpaka sasa ameipatia mabao mawili pekee katika mechi 12 alizozichezea tangu alipoanza kuwachezea mwezi Machi.

Tevez ambaye amewahi kuzichezea timu za Manchester United na Manchester City alijiunga na matajiri hao wa Shanghai kutoka Boca Juniors.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW